Tuesday, March 3, 2026
spot_img
HomeHabariWahamiaji 38 wakamatwa  Mbeya kwa kuingia nchini bila kibali

Wahamiaji 38 wakamatwa  Mbeya kwa kuingia nchini bila kibali

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu 38, akiwemo raia mmoja wa Ethiopia Tadesa Limoli (32) na wenzake 37 wote wanaume, kwa tuhuma za kuingia nchini kinyume cha sheria.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya SACP, Benjamin Kuzaga, watuhumiwa hao wamekamatwa Novemba 11, 2025 kwenye Pori la Ranchi ya Matebeteli wilayani Mbarali.

Ameeleza kuwa watu hao walikuwa wakisafiri kwa gari aina ya Toyota Noah lenye namba za usajili T.953DJF mali ya Stanslaus Mazengo mkazi wa Isitu, ambaye ndiye alikuwa akiendesha gari hilo.

“Uchunguzi wa awali umebaini kuwa Mazengo alikuwa akiwapeleka wahamiaji hao kwenye nyumba ya Jackline Malya (26), mkazi wa Chimala, kwa lengo la kuwahifadhi kabla ya safari ya kuwavusha kwenda Afrika Kusini kwa njia za zisizo rasmi,” amesema Kamanda Kuzaga.

Kutokana na tukio hilo, Kamanda Kuzaga ametoa wito kwa wananchi kuacha tamaa ya fedha inayowasukuma kushiriki vitendo vya kuwawezesha raia wa kigeni kuingia au kupita nchini bila kufuata taratibu za kisheria.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments