HomeBiasharaCRDB Insurance yasisitiza matumizi ya bima kwa usalama wa mali

CRDB Insurance yasisitiza matumizi ya bima kwa usalama wa mali

Upo Salama? Ni swali jepesi linaloulizwa na kampuni ya CRDB Insurance ikiwakumbusha Watanzania juu ya umuhimu wa kulinda mali ili kujihakikishia usalama wa mali kwa watu binafsi na wajasiriamali.

‎Akizindua kampeni hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Insurance, Wilson Mnzava amesema ‘Upo Salama?’ ni swali rahisi lakini lenye uzito mkubwa kwa kila mtu anayemiliki mali kwani ni muhimu kutanguliza usalama mahali popote unapokuwa iwe ni barabarani, nyumbani, kazini au kwenye biashara.

‎“Kwa muda mrefu, watu wengi wamekuwa wakitazama bima kama huduma inayotafutwa baada ya hasara kutokea au kutekeleza wajibu wa kisheria.

‎ Sisi CRDB Insurance Company tunaamini ni wakati wa kubadili mtazamo huo kwa kufahamu kwamba bima ni sehemu ya maisha ya kila siku, ni uwekezaji wa amani ya moyo, utulivu wa familia na mwendelezo wa biashara,” amesema Mnzava.

‎Kampeni hiyo inawakumbusha na kuwakumbusha wamiliki wa magari, nyumba na mali nyingine kukata bima kwa vitu wanavyovimiliki ili kuepuka hasara pindi inapotokea ajali, uharibifu mkubwa wa mali husika, wizi au changamoto nyingine zinazoweza kuathiri maisha ya watu na uwezo wao wa kujipatia kipato kutokana na mali wanazozimiliki.

‎Mnzava amewakumbusha Watanzania kuwa kampeni hii inalenga kuwakumbusha madereva wa magari binafsi, waendesha bodaboda, wasafirishaji wa bidhaa za biashara na watumiaji wote wa barabara kwamba usalama hauanzi pale tatizo linapotokea bali kabla ya hatari husika kutokea.

‎Akieleza kwa nini watu waitumie kampuni ya CRDB Insurance kwa mahitaji yao ya bima, Mnzava amesema wao ni mahiri katika kulipa fidia pindi mteja wao anapopata tatizo kwenye mali yake aliyoikatia bima na wakati wote wanahakikisha mteja anahudumiwa haraka ili kutositisha shughuli zake.

‎Kampuni ya CRDB Insurance imekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha matumizi ya bima za magari miongoni mwa wamiliki wa magari, kuwa kampuni ya kisasa na inayoelewa mahitaji halisi ya Watanzania katika kukuza na kuendeleza uchumi wao, pamoja na kujenga uhusiano wa kihisia kati ya wananchi na huduma za bima kwa kuzungumzia hali halisi wanazokutana nazo kila siku badala ya kuziangalia huduma za bima kama nyaraka au masharti ya kisheria pekee.

‎Kwa hatua inazochukua, kampuni ya CRDB Insurance inakusudia kuongeza ushiriki wa wananchi kupitia majukwaa ya kidijitali pamoja na kuhamasisha Watanzania kutembelea matawi ya Benki ya CRDB au kwenda kwa mawakala kupata elimu na huduma za bima.

‎Mnzava amesema “ahadi yetu ni kuendelea kutoa huduma za bima zinazopatikana kwa urahisi, zinazolipa madai kwa haki na kwa wakati, na zinazojengwa juu ya misingi ya uaminifu, uwazi na ukaribu na mteja.”

‎Sambamba na uzinduzi wa kampeni hiyo, kampuni ya CRDB Insurance imemtambulisha Hamisa Mobetto kuwa balozi atakayesaidia kufikisha elimu ya bima kwa wananchi.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments