Saturday, November 8, 2025
spot_img
HomeHabariDkt Samia: Nimetekeleza miradi yote iliyoanzishwa na Magufuli

Dkt Samia: Nimetekeleza miradi yote iliyoanzishwa na Magufuli

Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Samia Suluhu Hassan amesema katika kipindi cha miaka minne, Serikali yake imetekeleza miradi yote iliyoanzishwa na mtangulizi wake hayati John Magufuli mkoani Mwanza.

Miongoni mwa miradi hiyo, amesema ni ujenzi wa Daraja la JP Magufuli (Kigongo-Busisi), alilolikuta likiwa chini ya asilimia 30, lakini sasa linatumika. Magufuli aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, alifariki dunia Machi 17, 2021.

Dk. mia ameeleza hayo leo, Jumanne Oktoba 7, 2025 alipozungumza mbele ya wananchi wa Misungwi mkoani Mwanza, katika mkutano wake wa kampeni za urais.

Ameeleza baada ya kuapishwa kuwa Rais, alikwenda kujitambulisha mkoani Mwanza na kuahidi kuendeleza miradi iliyoanzishwa na Magufuli, jambo ambalo amelitimiza.

Mbali na Daraja la JP Magufuli, amesema pia ujenzi wa Meli ya MV Mwanza ulikuwa katika hatua ya mazungumzo, lakini sasa imekamilika na imeanza kufanyiwa majaribio.

Mbali na miradi hiyo, amesema hatua mbalimbali zimechukuliwa, kukidhi mahitaji ya maendeleo ya wananchi wa Misungwi mkoani Mwanza na Tanzania kwa ujumla.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments