📌 Yashika nafasi ya 11 mwaka 2025 kwa ongezeko la wageni wa kimataifa.
Bungeni-Dodoma: Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Ashatu Kijaji amesema Tanzania imefanikiwa kuwa miongoni mwa vinara duniani kwa ongezeko la watalii wa Kimataifa.
Akiwasilisha makadirio ya bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2026/2027 Bungeni Mjini Dodoma Dk. Kijaji amesema ongezeko hilo limefikia asilimia 7.1 kwa mujibu wa mizania ya dunia iliyofanywa na Shirika la Utalii duniani (UN Tourism).
“Naomba kumpongeza Mhifadhi na muongoza Watalii namba moja, Mheshimiwa Dk. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mchango mkubwa wa kuitangaza sekta ya utalii kimataifa hususani kwa kushiriki katika filamu ya “Tanzania The Royal Tour” na “Amaizing Tanzania” hatua ambayo imeasababisha ongezeko la Watalii nchini”. amesema Dk. Kijaji
Aidha, Dk. Kijaji ameongeza kuwa Tanzania imefanikiwa kuongeza idadi ya Watalii na kufikia watalii zaidi ya milioni 5.9 kwa mwaka 2025, ikiwa ni ongezeko la asilimia 10.7, ikilinganishwa na watalii milioni 5.3 kwa mwaka 2024 .









