HomeBiasharaTRA kujenga ofisi 49 kusogeza huduma karibu Kizimkazi

TRA kujenga ofisi 49 kusogeza huduma karibu Kizimkazi

Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omar, amesema Ofisi ya TRA Kizimkazi ni sehemu ya ofisi 49 zinazojengwa nchini na Kampuni ya CRJE ya China kwa gharama ya zaidi ya Sh bilioni 32, kwa lengo la kusogeza huduma za kodi karibu na wananchi na kuboresha mazingira ya ulipaji kodi.

Amesema Serikali imejipanga kuongeza utegemezi wa mapato ya ndani katika kugharamia miradi ya maendeleo, ambapo katika mwaka wa fedha 2026/2027 inatarajia kujitegemea kwa zaidi ya asilimia 74.

Waziri Omar ameagiza TRA kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA) kutumia miundombinu hiyo ili wananchi na wafanyabiashara wapate huduma kwa urahisi.

Aidha, amewataka wananchi na wafanyabiashara kulipa kodi kwa wakati, kwa ukamilifu na kwa hiari, akisisitiza kuwa mapato hayo ni muhimu katika kugharamia miradi ya maendeleo, ikiwemo barabara, nishati, maji, afya na elimu.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kusini, Othman Ali Maulid, amezitaka TRA na ZRA kuendelea kuimarisha ukusanyaji wa mapato sambamba na kutoa huduma bora na kusikiliza changamoto za wananchi na wafanyabiashara.

Naye mwakilishi wa wafanyabiashara wa sekta ya hoteli na utalii Zanzibar, Henry Kaunda, ameishukuru TRA na ZRA kwa ushirikiano wao na kuomba elimu zaidi ya mlipakodi iendelee kutolewa.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments