HomeHabariMiaka 30 jela kwa kumlawiti kijana mwenye changamoto ya akili

Miaka 30 jela kwa kumlawiti kijana mwenye changamoto ya akili

Mahakama ya Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya imemhukumu Amos Masanja (28), mkazi wa Igangwe, kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti kijana wa kiume mwenye umri wa miaka 20, ambaye jina lake limehifadhiwa.

Hukumu hiyo imetolewa Agosti 13, 2026 na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Chunya, Bruno Bungole.

Mahakama ilielezwa kuwa Masanja ametenda  kosa hilo Julai 7, 2026, katika Kitongoji na Kijiji cha Igangwe, Kata ya Mtanila, Tarafa ya Kipembawe, Wilaya ya Chunya.



Imedaiwa  kuwa mshitakiwa alimvuta mkono mhanga, ambaye ana changamoto za afya ya akili, na kuingia naye kwenye pagala ambako alimlawiti.

Wakati mshitakiwa akiendelea na kitendo hicho, watu waliokuwa wakipita karibu na eneo hilo walisikia sauti na kuingia ndani ya pagala hilo, ambapo walimkamata mshitakiwa na kumfikisha katika vyombo vya sheria.

Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Mwajabu Tengeneza, aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa ili iwe fundisho kwake na kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.

Baada ya kusikiliza ushahidi uliowasilishwa mahakamani, Hakimu Bungole alimhukumu Masanja kutumikia kifungo cha miaka 30 jela.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments