Timu ya wavu ya Korosho Queens imetangaza mpango wa kusajili wachezaji wapya wenye uzoefu mkubwa kuelekea mashindano yajayo.
Meneja wa timu hiyo, Hussein Kibombwe, amesema wameshaanza mazungumzo na wachezaji kadhaa ili kuimarisha kikosi.
“Tunataka kufanya usajili wa kishindo kwa kujenga timu imara zaidi msimu huu,” alisema Kibombwe.
Baada ya kumaliza nafasi ya nne kwenye Ligi Kuu ya Taifa ya Wavu, timu hiyo imetoa mapumziko mafupi kwa wachezaji wake wengi ambao ni wanafunzi walioko kwenye mitihani.
Korosho Queens pia imeishukuru Bodi ya Korosho Tanzania kwa kuendelea kuisaidia timu hiyo na kuwataka Watanzania kula korosho kwa wingi kwa afya bora.




