Saturday, November 8, 2025
spot_img
HomeHabariDC Msando apongeza DAWASA kwa utekelezaji wa mradi wa maji Ubungo

DC Msando apongeza DAWASA kwa utekelezaji wa mradi wa maji Ubungo

📍Dar es Salaam

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Albert Msando, amefanya ziara ya kukagua hali ya upatikanaji wa maji katika Wilaya hiyo, sambamba na kutembelea mradi wa maji wa King’ong’o unaotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), uliopo katika Kata ya Saranga.

Mradi huo unatarajiwa kuhudumia takribani wakazi 92,000 wa mitaa ya Michungwani, King’ong’o na Kimara B, na ni sehemu ya jitihada za serikali kuboresha huduma ya maji safi katika Jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya kukagua maendeleo ya mradi huo, Msando aliipongeza DAWASA kwa juhudi wanazoendelea kufanya katika kuhakikisha wananchi wa Ubungo wanapata huduma bora ya maji, akisisitiza umuhimu wa kukamilisha kazi hiyo kwa viwango vya juu na kwa wakati.

“Niipongeze DAWASA, lakini pia niishukuru Serikali kwa uwekezaji unaoendelea kufanyika katika sekta ya maji. Nitoe rai kwa wananchi kujenga utamaduni wa kuhifadhi maji ili kuepuka ukosefu wa maji pindi changamoto za kihuduma zinapojitokeza,” alisema Msando.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Modesta Mushi, alisema mradi huo unatekelezwa kwa ubora na kwa kuzingatia weledi wa hali ya juu, huku akiahidi kuwa kazi itakamilika ifikapo mwanzoni mwa Novemba 2025.

Katika ziara hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo pia alitembelea mitaa ya Tarakea na Kavimbilwa katika eneo la Mbezi Makabe, ambako alijionea hali nzuri ya upatikanaji wa maji na kuonesha kuridhishwa na huduma inayotolewa kwa wananchi.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments