Friday, May 15, 2026
spot_img
HomeHabariMV Kilindoni kurejesha safari za Mafia leo

MV Kilindoni kurejesha safari za Mafia leo

Baada ya hitilafu iliyojitokeza kwenye kivuko cha MV. Kilindoni kinachifanya safari zake Mafia kwenda Nyamisati na kusababisha usumbufu wa safari kwa wananchi kushindwa kusafiri kwa siku tatu hatimaye hali imerejea kawaida.

Kivuko hicho tayari kimetengenezwa na kinatarajiwa kuanza kutoa huduma tena rasmi kuanzia leo Mei 15.

Taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa  Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Gulam Dadikarim amesema taarufa kutoka kwa wahusika wa kivuko hicho tiketi zitaanza kuuzwa asubuhi na usiku safari ya kutoka Mafia kwenda Nyamisati itaanza.

Gulam amewapa pole wananchi wote kwa changamoto hiyo ya muda iliyojitokeza na kuahidi kuendelea kufuatilia kwa karibu huduma za usafiri ili kuhakikisha hawapati usumbufu wa mara kwa mara kutoka katika kituo hicho.

Pia amesema tayari kuna mipango ya kutafuta chombo kingine cha usafiri wa majini kitakachosaidia kuongeza huduma za usafiri kati ya Mafia na Nyamisati, hatua ambayo inalenga kupunguza changamoto za usafiri katika kisiwa hicho.

Naye Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mkoa wa Pwani Alvina Bushumba amekiri meli hiyo kurejea katika hali yake leo kwa safari za kutoka Mafia kwenda Nyamisati.

Bushumba amesema kwa siku ya leo meli hiyo itabeba watu na mizigo pekee hakutakuwa na magari yatakayovushwa  hadi pale kitakapokamilisha matengenezo.

Mmoja wa wananchi wa Mafia Omari Kapemba amethibitisha kuwepo kwa taarifa hizo zinazowawezesha wananchi kuendendelea na mipango ya safari kupitia meli hiyo.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments