Timu ya Taifa ya Vijana wa umri chini ya miaka 17 ya Senegal imetwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON U-17), baada ya kuifunga Tanzania (Serengeti Boys), penalti 4-2.
Huu ni ubingwa wa pili kwa Senegal katika michuano hiyo ya CAF.
Timu hizo zililazimika kwenda hatua ya matuta baada ya kumaliza dakika 90 Za kawaida wakiwa sare ya bao 1-1.
Bao la Serengeti Boys katika mechi hiyo lilifungwa na Hamisi Mahimbo dakika ya saba akiunganisha pasi fupi ya Luqman Mbalasalu.
Dakika ya 64, Ibrahima Dione, alifunga bao la kusawazisha baada ya kuwahi mpira uliookolewa na kipa wa Serengeti Boys, Haji Abdallah.
Senegal ilibeba ubingwa wa michuano hiyo kwa mara ya kwanza 2023.




