Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limethibitisha kuwakamata watuhumiwa wanne wote raia wa China kwa tuhuma za kuteka watu wawili raia wa China waliovamiwa katika majengo ya PSSSF, Ilala, Mei 14, 2026.
Wahanga hao ni, Weiyi Chen (64) na Liang Xiolo (44), walidaiwa kutekwa na kundi la wahalifu waliotumia magari yenye namba bandia huku wakitaka fidia ya dola milioni 20 za Kimarekani kutoka kwa ndugu zao.
Jeshi la Polisi lilifanikiwa kuwaokoa wahanga hao Mei 16, 2026 katika eneo la Mbezi, Kinondoni wakiwa wamejeruhiwa, ambapo walipelekwa katika Hospitali ya Agha Khan kwa matibabu, huku Weiyi Chen akiwa anaendelea kupatiwa matibabu kutokana na hali yake kutokuwa nzuri.
Watuhumiwa waliokamatwa katika operesheni hiyo ni Deng Anqing (49), Fan Zhong (49), Zhang Jianjun (51) na Deng Qiang (40), pamoja na magari mawili yaliyodaiwa kutumika kwenye tukio hilo yalitiwa nguvuni pamoja na vielelezo mbalimbali.
Jeshi la Polisi limesema linaendelea na uchunguzi zaidi ili kuwabaini wahusika wengine wote waliohusika kuwashukuru wananchi ambao wamekuwa wakitoa taarifa za kweli ambazo zimesaidia kuzuia uhalifu na zingine kuwakamata wanaojihiusisha na vitendo vya kihalifu.






