Thursday, May 7, 2026
spot_img
HomeElimuWaziri Mkenda ataja mikakati ya kuboresha elimu

Waziri Mkenda ataja mikakati ya kuboresha elimu


Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia imesema itaendelea kuimarisha sekta ya elimu katika ngazi zote kuanzia elimu ya awali, msingi, sekondari hadi elimu ya juu kupitia uwekezaji mkubwa wa miundombinu, mafunzo na ubora wa ufundishaji. 

Hayo yamesemwa bungeni Jijini Dodoma na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/2027.

Prof.Mkenda amesema  katika mwaka wa fedha 2026/27, Serikali imepanga kujenga madarasa 1,360 ili kusaidia utekelezaji wa sera ya elimu ya miaka 10 ya lazima, pamoja na kujenga mabweni 17 katika shule za sekondari na nyumba 33 za walimu ili kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia. 

” Serikali itaendelea kuboresha ubora wa elimu kwa kufanya tathmini katika taasisi zaidi ya 7,000 za elimu nchini pamoja na kuimarisha ofisi za uthibiti ubora wa shule katika baadhi ya maeneo ya kimkakati.”amesema. 

Prof.Mkenda amesema mkazo pia utawekwa katika kuimarisha stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa kuwajengea uwezo walimu zaidi ya 1,300 kutumia mbinu bunifu za ufundishaji.

Aidha, Serikali itaendelea kuimarisha taaluma ya ualimu kupitia mafunzo ya vitendo kwa walimu tarajali, pamoja na kutoa ufadhili wa masomo kwa walimu zaidi ya 1,200 na mafunzo ya stadi mbalimbali kwa  watumishi wa sekta ya elimu.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments