Wednesday, February 4, 2026
spot_img
HomeHabariDk.Rais Samia anavyoitangaza Tanzania Duniani

Dk.Rais Samia anavyoitangaza Tanzania Duniani

Rais, Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania imepanda nafasi tisa katika orodha ya mataifa yanayotajwa kuwa vituo bora vya uwekezaji duniani, akiwahakikishia wawekezaji kuwepo kwa miundombinu bora ya kukuza biashara.

Dk.Samia ametoa kauli hiyo usiku wa kuamkia leo, Jumatano Februari 4, 2026 alipozungumza katika uzinduzi wa Jukwaa la Uwekezaji Duniani kwa upande wa Afrika (GAIS), linalofanyika Dubai, katika Taifa la Falme za Kiarabu.

“Wawekezaji mliopo hapa, niwahakikishie mambo matatu (Tanzania). Kuna miundombinu bora ya barabara na reli ya kisasa. Kwa ujumla Tanzania tayari ina uti wa mgongo wa ukuzaji biashara,” amesema.

Sambamba na hayo, amesema Tanzania pia imetenga maeneo kwa ajili ya uwekezaji, ambayo mwekezaji atapatiwa kibali na cheti cha kutumia ardhi ya kuwekeza na nafuu ya kodi, huduma zote hizo kupitia kituo cha huduma za pamoja, kuhakikisha michakato rahisi na haraka.

“Pia, (Tanzania) kuna Serikali inayotenda kulingana na inachosema. Tanzania tunafanyia kazi tunachokipanga. Wawekezaji kwa sasa hawatafuti fursa pekee, bali wanatafuta uhakika wa sera zinazotabirika, taasisi na washirika wa uhakika na Tanzania ni mshirika sahihi katika hayo,” amesema.

Amesema Tanzania inathamini uhusiano unaojengwa kwa uwajibikaji, heshima na maslahi kwa pande zote, akiwaalika wawekezaji kuingia nchini kushuhudia fursa mbalimbali zilizopo na kuona maeneo wanayoweza kushirikiana kwa maslahi yao na Watanzania.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments