Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ametaka mbali na vyumba vya kunyonyeshea katika Soko la Kariakoo, kujengwe vyumba vya malezi ya watoto, kwa kuishirikisha sekta binafsi, ili mama zao wanaofanya biashara wapate muda wa kufanya shughuli zao.
Samia ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam leo, Jumapili Februari 8, 2026 alipofungua Soko la Kariakoo lililojengwa upya baada ya kuungua mwaka 2021.
“Ninyi (uongozi wa soko) mtatoa eneo, lakini akitokea mtu binafsi kuweka kitengo hicho cha kulea watoto ambacho kitaangaliwa vizuri, vifaa vyote, watoto watakula vizuri, sekta binafsi karibuni,” amesema.
Amependekeza mbali na vyumba vya kunyonyeshea, kuwe na eneo la kulea watoto ambao mama zao watakua wanafanya biashara.




