Saturday, April 25, 2026
spot_img
HomeHabariPSSSF yashiriki Maonesho ya OSHA 2026 Njombe

PSSSF yashiriki Maonesho ya OSHA 2026 Njombe

‎Njombe Aprili 25, 2026-Maonesho ya Wiki ya Afya na Usalama mahali pa Kazi Kitaifa, yameanza kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Mji Mwema mkoani Njombe ambapo taasisi mbalimbali ikiwemo PSSSF zinatoa huduma kwa wananchi wanaotembelea maonesho hayo kuanzia Aprili 24-28, 2026.

‎Akizungumza kwenye maonesho hayo yaliyobeba kaulimbiu isemayo “Mazingira Bora ya Kisaikolojia na Kijamii Kazini ni Njia ya Kuimarisha Ustawi wa Wafanyakazi na Kujenga Taasisi imara,” Afisa Mfawidhi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Mkoani Njombe Andrew Dayson, amewakaribisha wanachama na wananchi ili kupata huduma mbalimbali zinazotolewa na PSSSF lakini hasa kupata elimu na ufafanuzi kuhusu maboresho ya huduma na mafao yanayotolewa na Mfuko.

‎Alisema, Maonesho hayo ni fursa nzuri ya PSSSF kukutana na wanachama na wananchi sio tu kuwahudumia lakini pia kuwapatia elimu ya matumizi ya teknolojia ili waweze kujihudumia wao wenyewe popote walipo kupitia PSSSF Kidijitali.

‎Naye Afisa Uhusiano PSSSF, Jackline Jackson, amedokeza kuwa katika PSSSF Kidijitali, mwanachama anaweza kupata taarifa za michango, taarifa za mafao, kuwasilisha madai mbalimbali, kuhuwisha taarifa za wategemezi na kwa wastaafu wanaweza kujihakiki kupitia simu janja.

‎“Pia tunawakaribisha sana ili mpate taarifa kuhusu fursa mbalimbali za kiuchumia zinazopatikana PSSSF kupitia uwekezaji wake kwenye viwanda na majengo.” Alisisitiza.

‎Naye mwanachama wa PSSSF Mwalimu Brown Ulaya kutoka shule ya Msingi Ihalula, Halmashauri ya Mji wa Njombe ambaye alifika kwenye banda la PSSSF kuhudumiwa, alisema pamoja na kuona michango yake lakini pia ameelimishwa kuhusu namna anavyoweza kujihudumia mwenyewe kupitia simu janja.

‎“ Lakini pia nilitaka kujua utaratibu wa kustaafu kabla ya miaka 60, nashukuru kuwa nilipata ufafanuzi kuwa kuna mtumishi anaruhusiwa kustaafu kwa hiari piandi anapofikisha miaka 55.” Alisema.


RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments