Saturday, April 25, 2026
spot_img
HomeBiasharaDkt Samia: Tunaiunganisha sekta ya uvuvi na viwanda, masoko

Dkt Samia: Tunaiunganisha sekta ya uvuvi na viwanda, masoko

Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, amesema uzinduzi wa boti mpya ya uvuvi wa bahari kuu, ni mpango na mfumo unaounganisha uvuvi, uzalishaji viwandani na masoko.

‎Mkuu huyo wa nchi, ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam leo, Jumamosi Aprili 25, 2026 alipozungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa meli ya kwanza ya uvuvi wa bahari kuu.

‎Amesema ni muhimu kutambua mafanikio ya sekta ya uvuvi hayategemei kuwepo kwa meli hiyo pekee, bali Serikali inajenga miundombinu zikiwemo bandari za uvuvi na viwanda vya kuchakata mazao ya uvuvi.

‎“Hatua hizi, zinalenga kupanua uzalishaji fursa za kiuchumi, ajira kwa wananchi pamoja na kuimarisha usalama wa chakula kwa sababu mazao ya baharini ni lishe na lishe muhimu sana,” amesema.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments