Simba imebeba ubingwa wa mashindano ya Kombe la Muungano 2026 baada ya kuifunga Yanga bao 1-0.
Selemani Mwalimu aliifungia Simba bao hilo la ushindi kwa penalti na kumaliza “unyonge” kwa watani zao ambao waliwafunga katika mechi tano mfululizo.
Mechi hiyo ililazimika kuongezwa dakika 30 baada ya dakika 90 Za kawaida timu hizo za Kariakoo kutokufungana.
Kocha wa Simba, Steve Barker ametangazwa kuwa Kocha Bora wa mashindano hayo huku tuzo wa Mchezaji Bora wa michuano hiyo ikienda kwa beki wa Wekundu wa Msimbazi, Rushine de Reuck.
Kwa ushindi huo, Simba atapewa zawadi ya Sh.milioni 150.




