Wednesday, May 6, 2026
spot_img
HomeHabariRais Samia: Tumepeleka zaidi ya vijana 7,000 kufanya kazi nje

Rais Samia: Tumepeleka zaidi ya vijana 7,000 kufanya kazi nje

Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali yake imeshapeleka vijana zaidi ya 7,000 kufanya kazi nje ya nchi, akisisitiza haki na stahiki zao zikasimamiwe vema.

Mkuu huyo wa nchi, amemwagiza Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Uhusiano, Dk Everlyne Munisi, kwa kushirikiana na wenzake alitimize hilo.

Dkt Samia ameyasema hayo Ikulu jijini Dodoma leo, Jumatano Mei 6, 2026 alipozungumza baada ya kuwaapisha viongozi kadhaa aliowateua.

Amesema Serikali yake ilishaanza kutafuta ajira za vijana nje ya nchi, kwa muda mrefu zilikuwa zinapatikana nafasi lakini ndani ya wizara kulikuwa na tatizo.

“Mwaka huu tumeanza kufungua, tumeshapeleka zaidi ya vijana 7,000 nje, wasimamiwe haki, mawakala wasimamiwe, haki zao kule na sheria za kazi, Serikali za kule zifuate sheria zao, lakini na vijana wetu waende wakafuate sheria za watu na stahiki za vijana wetu zikapatikane,” amesema.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments