HomeMichezo‎Senegal mabingwa fainali AFCON U-17 2026

‎Senegal mabingwa fainali AFCON U-17 2026

Timu ya Taifa ya Vijana wa umri chini ya miaka 17 ya Senegal imetwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON U-17), baada ya kuifunga Tanzania (Serengeti Boys), penalti 4-2.

‎‎Huu ni ubingwa wa pili kwa Senegal katika michuano hiyo ya CAF.‎‎

Timu hizo zililazimika kwenda hatua ya matuta baada ya kumaliza dakika 90 Za kawaida wakiwa sare ya bao 1-1.‎‎

Bao la Serengeti Boys katika mechi hiyo lilifungwa na Hamisi Mahimbo dakika ya saba akiunganisha pasi fupi ya Luqman Mbalasalu.‎‎

Dakika ya 64, Ibrahima Dione, alifunga bao la kusawazisha baada ya kuwahi mpira uliookolewa na kipa wa Serengeti Boys, Haji Abdallah.‎‎

Senegal ilibeba ubingwa wa michuano hiyo kwa mara ya kwanza 2023.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments