HomeHabariMarekani yaipa Tanzania nafasi ya kuanza mchakato wa mageuzi

Marekani yaipa Tanzania nafasi ya kuanza mchakato wa mageuzi

Bunge la Seneti la Marekani limefanya mabadiliko katika Muswada wa Mapitio ya Uhusiano wa Uwili kati ya Marekani na Tanzania kwa kulegeza masharti kuhusu hatua zinazotakiwa kuchukuliwa na Tanzania katika mageuzi ya mifumo ya uchaguzi na utawala.

‎Katika rasimu ya awali ya muswada huo, Tanzania ilitakiwa kutekeleza moja kwa moja mabadiliko ya sheria na mifumo ya uchaguzi zilizotajwa na Marekani, huku rasimu iliyopitishwa Juni 17, 2026 imetaka utekelezwaji wa hayo uanze na mchakato.

Mabadiliko hayo yanaonyesha kutambuliwa kwa ukweli kwamba baadhi ya mageuzi yanahitaji muda na hatua mbalimbali.

Hatua hiyo inaonekana kutoa nafasi zaidi kwa Tanzania kuonyesha dhamira ya kushughulikia mabadiliko hayo. Pia, inafungua uwezekano wa kuendelea kwa mazungumzo na ushirikiano wakati mchakato wa utekelezaji ukiendelea.

Muswada huu unapatikana katika tovuti ya Bunge la Seneti la Marekani

https://www.foreign.senate.gov/imo/media/doc/de7611cb-ee2e-13e6-805f-4cd0d6deb584/S.4577_Managers_Substitute_Amendment_6ff7d3a2-5190-4fc6-ac7e-5fc73255f73e.pdf

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments