
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametembelea banda la vijana katika kilele cha Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima ya Kimataifa ya Nanenane, yaliyofanyika leo Agosti 8, 2026, katika Viwanja vya Dkt. John Malecela, Nzuguni, jijini Dodoma.




Akiwa katika banda hilo, Rais Samia amepata fursa ya kusikiliza na kujionea kazi mbalimbali za ubunifu zinazofanywa na vijana wanaotekeleza Mradi wa Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT), kupitia fursa zinazotolewa na Serikali katika sekta ya kilimo.
Ziara hiyo imeonesha namna vijana wanavyotumia fursa zinazotolewa na Serikali kuwekeza katika kilimo, ubunifu na shughuli nyingine za uzalishaji, hatua inayolenga kuongeza ajira, kipato na mchango wao katika maendeleo ya uchumi wa Taifa.






