HomeGeneral NewsPSSSF: Tutaendelea kutoa huduma bora na za haraka

PSSSF: Tutaendelea kutoa huduma bora na za haraka

Dodoma, Agosti 8, 2026: Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), umewahakikishia wanachama na wastaafu kuwa Mfuko huo utaendelea kuboresha na kutoa huduma bora, za haraka na zenye uhakika.

Hayo ameyasema Meneja wa PSSSF Kanda ya Kati, Bw. Sayi Lulyalya, wakati akitoa shukrani kwa Wanachama, Wastaafu na Wananchi waliotembelea katika mabanda ya PSSSF wakati wa Maonesho ya Kilimo na Uvuvi (Nanenane) yaliyofikia kilele Agosti 8, 2026.

Mgeni rasmi katika sherehe za ufungaji maonesho hayo kitaifa jijini Dodoma alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Bw. Sayi aliwashukuru Wanachama na Wananchi waliotembelea banda la PSSSF katika Maonesho ya Kilimo na Uvuvi (Nanenane) hapa Dodoma, lakini pia Kanda ya Magaribi Mkoani Tabora, Kanda ya Kusini Mkoani Lindi, Kanda ya Nyanda za Juu Mkoani Mbeya, Kanda ya Ziwa Magaribi Mkoani Mwanza, lakini pia Zanzibar.” Alisema.

“ Tunathamini mwitikio wa wananchi na wanachama waliotembelea banda la Mfuko na kupata huduma pamoja na elimu kuhusu masuala mbalimbali ya hifadhi ya jamii; Tunaahidi kuendelea kutoa huduma bora, za haraka na zenye uhakika kwa wanachama na wastaafu,” alisema.

Amewasihi wanachama na wastaafu kuendelea kutumia mifumo ya kidijitali, ikiwemo PSSSF Portal, ili kupata huduma kwa urahisi na kwa wakati bila ulazima wa kufika ofisini.

“ Hivi sasa tumerahisisha upatikanaji wa huduma ikijumuisha Wanachama kupata Taarifa za Mafao, Kuwasilisha madai mbalimbali, Kuhuwisha Taarifa za Wategemezi na Wastaafu nao wanaweza Kujihakiki kupitia simu janja.

Kutokana na kuboresha mifumo yetu PSSSF imeweza kulipa mafao kwa wakati na ndio maana tuna kauli mbiu yetu tunayosema TUNALIPA JANA MSTAAFU WA LEO na kauli hii tunaitekeleza kwa vitendo, alisisitiza Bw. Lulyalya.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments