HomeAfyaMUHAS yaonyesha bunifu nane kutatua changamoto za jamii

MUHAS yaonyesha bunifu nane kutatua changamoto za jamii

Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kimeonyesha bunifu zalishi nane katika Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu, zinazolenga kutatua changamoto katika afya, kilimo na ustawi wa jamii.

Miongoni mwa bunifu hizo ni ROBOSPINE, inayosaidia watoto wenye spina bifida kusimama, kutembea na kufanya mazoezi; BILIMEASURE, inayopima kiwango cha bilirubin kwa watoto wachanga bila kuchukua damu; na SIKUSMART, inayotabiri mzunguko wa hedhi na kipindi cha yai kupevuka bila kuhitaji simu janja au intaneti.

Bunifu nyingine ni BRIDGING SILENCE, inayotumia Akili Bandia (AI) kutafsiri lugha ya alama kuwa maandishi na sauti ya Kiswahili; BIOSAFE, kiuatilifu hai cha asili kinachosaidia kudhibiti magonjwa ya mimea; MoyoGuard, inayorekodi mapigo ya moyo ndani ya sekunde 30 bila intaneti; pamoja na QR DHARURA, inayorahisisha upatikanaji wa taarifa muhimu za mtu wakati wa dharura.

Kupitia bunifu hizo, MUHAS inaendelea kuunganisha elimu, utafiti na teknolojia katika kutengeneza suluhisho zinazolenga kuboresha afya, kukuza ujumuishi, kulinda mazingira na kuongeza ustawi wa jamii.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments