HomeHabariRais Samia kwenda Zambia kushiriki uapisho Hichilema

Rais Samia kwenda Zambia kushiriki uapisho Hichilema

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameondoka Zanzibar kuelekea nchini Zambia kushiriki sherehe za kuapishwa kwa Rais mteule wa Zambia, Hakainde Hichilema.

Rais Samia ameondoka leo, Septemba 1, 2026, kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Zanzibar, ambapo ameagwa na viongozi mbalimbali.

Sherehe za uapisho wa Rais Hichilema zinatarajiwa kufanyika nchini Zambia, huku viongozi mbalimbali kutoka ndani na nje ya Afrika wakitarajiwa kuhudhuria.

Ziara hiyo ya Rais Samia inaendelea kuonesha ushirikiano na uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Zambia.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments