HomeHabariJaji Warioba adondoka ghafla akihutubia mkutano wa hali ya kisiasa

Jaji Warioba adondoka ghafla akihutubia mkutano wa hali ya kisiasa

Makamu wa Rais na Waziri  Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba, amedondoka ghafla wakati akihutubia Mkutano wa Kitaifa wa kujadili  hali  ya kisiasa nchini, Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 na mustakabali wa Taifa unaofanyika jijini Dar es Salaam

‎Jaji Warioba alikuwa akizungumza katika mkutano huo ulioandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania  (TCD), ambapo alikuwa ni mgeni rasmi.

‎Tukio hilo limetokea wakati Jaji Warioba akieleza hoja mbalimbali kuhusu hali ya kisiasa nchini, huku akisisitiza masuala yanayohusu mustakabali wa taifa na umuhimu wa kujenga mazingira yanayolinda demokrasia.

‎Baada ya kuanguka, watu waliokuwa karibu naye walimsaidia na kumtoa ukumbini kwa  ajili ya kupatiwa msaada.

‎Mwenyekiti wa TCD, Dorothy Semu,amewaambia washiriki hali ya Jaji Warioba imetengamaa na amekwenda kupumzika.

Chanzo: Nipashe Digitali

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments