Friday, December 19, 2025
spot_img
HomeMichezoAzam FC yamtambulisha straika wa CHAN

Azam FC yamtambulisha straika wa CHAN

Klabu ya Azam FC imemtambulisha rasmi mshambuliaji Jephte Kitambala Bola kutoka AS Maniema ya DR Congo kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Kitambala, ambaye yupo kwenye kikosi cha taifa cha DR Congo kinachoshiriki fainali za CHAN nchini Kenya na Uganda, amecheza michezo yote ya Kundi A dhidi ya Kenya na Zambia.

Azam tayari imesajili nyota wengine akiwemo Aishi Manula kutoka Simba, Himid Mao kutoka Ghazl El Mahalla ya Misri, Pape Doudou Diallo kutoka Senegal, beki Lameck Lawi kutoka Coastal Union na Muhsin Malima kutoka klabu ya Zed nchini Misri.

Aidha, zipo taarifa kuwa Azam ipo hatua za mwisho kumsajili kiungo mkabaji wa zamani wa Simba, raia wa Mali, Sadio Kanoute, ambaye aliichezea Simba kuanzia 2021 hadi 2024 kabla ya kujiunga na JS Kabylie ya Algeria.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments