Wachezaji wa safu ya ulinzi wa Yanga Princess, Diana Mnally na Mnigeria Igwe Uzoamaka, wametia saini mikataba mipya ya miaka miwili.

Hatua hiyo inakuja baada ya tetesi kuwa nyota hao walikuwa sokoni.
Yanga Princess chini ya Kocha Edna Lema inalenga kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu mpya, ikisaka mafanikio baada ya kushindwa kutwaa ubingwa msimu uliopita uliokwenda kwa JKT Queens.




