Monday, March 9, 2026
spot_img
HomeMichezoTanzania yapangwa Kundi A Kombe la Dunia Kabbadi

Tanzania yapangwa Kundi A Kombe la Dunia Kabbadi

Tanzania imepangwa Kundi A kwenye Kombe la Dunia la Kabbadi ya ufukweni ikikabiliana na Malaysia, Hungary na China. Mashindano hayo yatafanyika Septemba 23–29, 2025 kwenye fukwe za Port Dickson, Malaysia.

Mwenyekiti wa Chama cha Kabbadi Tanzania, Abdalah Nyoni, amesema kikosi kinaendelea na mazoezi katika Viwanja vya Mwembe Yanga, huku kambi rasmi ikitarajiwa kuanza Septemba 8 katika Chuo Kikuu cha Kimataifa Kampala, Gongo la Mboto.

Nyoni alisisitiza lengo ni kushinda michezo yote na kuomba wadau kujitokeza kusaidia wachezaji na viongozi kifedha ili kufanikisha maandalizi ya safari hiyo.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments