Friday, November 14, 2025
spot_img
HomeHabariBashiru: Dkt Samia ameshinda majaribu, tutavuka salama

Bashiru: Dkt Samia ameshinda majaribu, tutavuka salama

Katibu Mkuu mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Bashiru Ally amesema Mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho, Dkt Samia Suluhu Hassan amekunda na majaribu, ameyashinda majaribu hivyo ataivusha nchi salama.

Amesema kupitia uongozi wa Dkt Samia, nchi imebaki moja, chama chenye umoja na amani imetamalaki, ingawa aliingia katikati ya kipindi kigumu cha mabadiliko ya ghafla ya Serikali.

Dk Bashiru ametoa kauli hiyo leo, Jumatano Oktoba 8, 2025 alipozungumza katika mkutano wa kampeni za urais, uliofanyika katika Uwanja wa Nyamagana mkoani Mwanza.

“Nasikia maneno kutoka kwa vijana kana kwamba kuna wasiwasi hivi. Nawahakikishia huyu kiongozi wetu ambaye anaomba ridhaa tena, amekutana na majaribu, ameshajaribiwa na ameshinda majaribu na tuna uhakika tutavuka salama,” amesema.

Amesema kama nchi imebaki moja, chama kimoja, usalama na amani umetamalaki tena katika kipindi kigumu cha mabadiliko ya Serikali ya ghafla, rabsha zinazopangwa Dkt Samia anamudu kuzidhibiti.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments