Friday, November 14, 2025
spot_img
HomeHabariDkt Samia: Kwa SGR Mwanza-Dar tutasafiri kwa saa nane

Dkt Samia: Kwa SGR Mwanza-Dar tutasafiri kwa saa nane

Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Samia Suluhu Hassan amesema baada ya kukamilisha utekelezaji wa mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) na kuunganisha Mkoa wa Mwanza na Dar es Salaam, safari kwa njia hiyo itakuwa ya saa nane.

Hatua hiyo, itapunguza mara mbili zaidi ya muda wa safari unaotumika sasa kwa njia ya barabara, ambayo nis aa 18 kutoka Mwanza hadi Dar es Salaam.

Dk Samia ameyasema hayo leo, Jumatano Oktoba 8, 2025 alipozungumza na wananchi wa Nyamagana mkoani Mwanza, katika mkutano wake wa kampeni za urais.

Amesema kwa sasa Serikali yake inaendelea na utekelezaji wa kipande cha reli hiyo cha Mwanza-Isaka chenye urefu wa kilomita 314, kwa gharama ya Sh3 trilioni na tayari kimefikia asilimia 63.

Amesema mkoa huo utakuwa na stesheni tano za abiria, Mwanza Mjini, Fela, Mantare, Bukimbwa na Mallya, zitakazoshusha na kupakia abiria.

Katika stesheni hizo, amesema anatarajia kutakuwa na shughuli za kiuchumi yakiwemo malazi, hivyo ni jukumu la wakazi wa Mwanza kuchangamkia fursa.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments