Saturday, November 8, 2025
spot_img
HomeGeneral NewsDk. Ntuli ashinda kwa kishindo Ukurugenzi Mkuu wa ECSA-HC

Dk. Ntuli ashinda kwa kishindo Ukurugenzi Mkuu wa ECSA-HC

Mkurugenzi wa Kinga wa Wizara ya Afya kutoka Tanzania Dk. Ntuli Kapologwe, ameibuka mshindi wa nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Jumuiya ya Afya ya Nchi za Afrika Mashariki, Kati, na Kusini (ECSA – HC) na kuwashinda wagombea wengine sita waliokuwa wakiwania nafasi hiyo.

Dk. Ntuli  anachukua nafasi hiyo kutoka kwa Prof. Yoswa Dambisya wa Uganda ambaye amehudumu kwenye nafasi hiyo  kwa mihula miwili ndani ya miaka 10.

Dk. Ntuli Kapologwe kwa kuzingatia vigezo maalum vilivyowekwa katika makubaliano ya Jumuiya hiyo,  ataongoza kwa muda wa miaka mitano. 

Akizungumza mara baada ya kuhitimisha zoezi la uchaguzi Februari 12, 2025, Waziri wa Afya nchini Tanzania  Jenista Mhagama amesema kuwa nafasi hiyo ilipotangazwa kwa mara ya kwanza  jumla ya waombaji 47 waliwasilisha wasifu wao na kati yao, saba  walichaguliwa kuendelea baada ya mchujo wa awali.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments