Sunday, November 9, 2025
spot_img
HomeHabariDkt Samia: Mimi ni mama, naomba ridhaa nitawalea

Dkt Samia: Mimi ni mama, naomba ridhaa nitawalea

Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan amesema kwa kuwa yeye ni mama ataendelea kuwalea wananchi kwa kuhakikisha anafanikisha shughuli zitakazoinua maisha yao.

Miongoni mwa aliyoyafanya kuinua maisha ya wananchi, Dk. Samia amesema ni kuwawekea mazingira wachimbaji wadogo hasa vijana wanufaike na sekta ya madini.

Dk. Samia ametoa kauli hiyo leo, Jumapili Oktoba 12, 2025 alipozungumza katika mkutano wa kampeni za urais, uliofanyika Bukombe mkoani Geita.

Jambo lingine linaloashiria malezi kwa wananchi, amesema Serikali yake inatoa ruzuku ya mbolea na pembejeo kuhakikisha wakulima wanalima zaidi na kupata mavuno mengi ili wanufaike kiuchumi.

Kama ilivyo katika sekta ya kilimo, amesema ndivyo ilivyo kwa mifugo ambako Serikali imeanza kutoa ruzuku ya chanjo na inalenga kuanzisha viwanda vya kuchakata maziwa na kuwanufaisha wafugaji.

“Tunaposema kazi na utu tunadhamiria. Tufanye kazi, tuulinde, tuujenge na tuuimarishe utu wa Mtanzania na utu wa Mwana Bukombe,” amesema.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments