HomeBiasharaNMB yasogeza huduma kamili za kibenki kwa wananchi Sabasaba

NMB yasogeza huduma kamili za kibenki kwa wananchi Sabasaba

DAR ES SALAAM: Wakazi na wageni wa Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara (DITF) sasa wanapata huduma za kibenki ndani ya Viwanja vya Saba Saba kupitia Tawi la NMB Saba Saba, linalofanya kazi kuanzia Juni 28 hadi Julai 13, 2026.

Tawi hilo linatoa huduma za kufungua akaunti, kuweka na kutoa fedha, malipo ya Serikali, bima na huduma za kidijitali, pamoja na ATM na mawakala waliopo viwanjani.

Kaimu Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, William Nkuna, alisema tawi hilo linalenga kusogeza huduma karibu na wananchi na wafanyabiashara wanaohudhuria maonesho.

Pia, NMB inatoa ushauri wa mikopo na huduma za kidijitali, huku wateja wakipata mikopo ya hadi Sh milioni 2 na wafanyabiashara hadi Sh milioni 5 kupitia simu.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments