Friday, December 5, 2025
spot_img
HomeMichezoSingida Black Stars waapa ‘kuzima moto’ wa Pamba Jiji Mwanza

Singida Black Stars waapa ‘kuzima moto’ wa Pamba Jiji Mwanza

Kikosi cha Singida Black Stars kimetua salama jijini Mwanza kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Pamba Jiji FC, utakaochezwa keshokutwa kwenye Uwanja wa CCM Nyamagana.

Msemaji wa timu hiyo, Hussein Massanza, alisema wachezaji wako kwenye morali ya juu na wamejiandaa kikamilifu kuendeleza ushindani waliouonyesha kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.

Alisema licha ya kutarajia mchezo mgumu, malengo yao ni kuibuka na pointi tatu muhimu wakiwa ugenini.
“Tutaingia kwa umakini mkubwa. Tunahitaji kuendeleza moto uleule na kurudi nyumbani na ushindi,” alisema.

Singida Black Stars ni miongoni mwa timu mbili za Tanzania, pamoja na Azam FC, zilizofuzu hatua ya makundi ya mashindano hayo ya CAF Confederation Cup.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments