Wednesday, April 29, 2026
spot_img
HomeBiasharaCRDB yavunja rekodi faida robo ya kwanza ya mwaka 2026

CRDB yavunja rekodi faida robo ya kwanza ya mwaka 2026

CRDB Bank Plc imeendelea kuonyesha uimara wa kifedha baada ya kurekodi faida baada ya kodi ya Shilingi bilioni 206 katika Robo ya Kwanza ya mwaka 2026, ikiwa ni ongezeko la asilimia 18.9 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka uliopita.

Matokeo hayo yanaifanya benki hiyo kuongoza katika viashiria muhimu vya kifedha na kiutendaji, huku mizania yake ikiendelea kuimarika. Jumla ya mali za benki imeongezeka kwa asilimia 7.1 na kufikia Shilingi trilioni 23.9, wakati mikopo kwa wateja ikikua kwa asilimia 6.8 hadi Shilingi trilioni 14.7.

Aidha, amana za wateja zimeongezeka kwa asilimia 9 na kufikia Shilingi trilioni 16.3, hatua inayoashiria kuongezeka kwa imani ya wateja kwa benki hiyo.

Akizungumzia mafanikio hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Abdulmajid Mussa Nsekela, alisema ongezeko la faida ni matokeo ya utekelezaji madhubuti wa mkakati wa biashara unaolenga kuongeza thamani kwa wateja na kuchochea ukuaji wa uchumi.

Aliongeza kuwa mafanikio hayo pia yanatokana na juhudi za benki katika kuimarisha huduma, kupanua wigo wa kifedha na kuhakikisha wanahisa wanapata thamani endelevu.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments