Rais wa Marekani Donald Trump amebariki uteuzi wa Darline Graham Nordone, dada wa aliyekuwa Seneta wa Marekani Lindsey Graham, kuchukua nafasi yake baada ya mwanasiasa huyo wa jimbo la South Carolina kufariki dunia Julai 11, 2026.
Gavana wa South Carolina, Henry McMaster, alitangaza uteuzi huo jana Jumatatu na kumtambulisha Nordone kama “dada mdogo mpendwa” wa Graham, akisema atakamilisha kazi iliyoachwa na seneta huyo.
“Ni heshima kubwa sana. Lindsey amekuwa akinisaidia siku zote, na sasa nami nitakuwa kwa ajili yake,” alisema Nordone baada ya kutangazwa rasmi.


Uteuzi huo unafuatia wito wa viongozi mbalimbali, akiwamo Rais Trump, waliomtaka Nordone kushika nafasi hiyo kama sehemu ya kumuenzi Graham, ambaye hakuwahi kuoa wala kupata watoto.
Lindsey Graham alikuwa mshirika wa karibu sana wa Rais Trump na mmoja wa wanasiasa waliokuwa na ushawishi mkubwa ndani ya duru za kisiasa za chama chake. Uhusiano wao wa karibu uliifanya Graham kuwa miongoni mwa wanasiasa waliounga mkono kwa kiasi kikubwa ajenda mbalimbali za utawala wa Trump.
Kwa mujibu wa Gavana McMaster, Nordone atahudumu katika nafasi hiyo hadi mwisho wa muhula wa Graham unaotarajiwa kumalizika mwaka 2027.






