HomeBiasharaRais Mwinyi:  Hongereni Benki ya CRDB kwa kuchochea maendeleo, kukuza uchumi

Rais Mwinyi:  Hongereni Benki ya CRDB kwa kuchochea maendeleo, kukuza uchumi

Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameipongeza CRDB Bank kwa mchango wake mkubwa katika kuchochea maendeleo ya kiuchumi, kuwezesha utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuwawezesha vijana kiuchumi kupitia huduma na bidhaa za fedha inazotoa.

Dkt. Mwinyi aliyeambatana na mkewe, Mariam Mwinyi ametoa pongezi hizo alipotembelea tawi la Benki ya CRDB lilipo ndani ya Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere maarufu kama Sabasaba kabla hajatangaza kufungwa kwa Maonyesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF).

Baada ya hafla ya kufunga maonesho hayo, alitembelea banda la CRDB Bank na kupata fursa ya kujionea huduma mbalimbali za kibunifu zinazotolewa na benki hiyo kwa wananchi, wafanyabiashara na wawekezaji.

Rais Mwinyi amesema Benki ya CRDB imeendelea kuwa mshirika muhimu wa maendeleo kwa kutoa suluhisho za kifedha zinazowezesha ukuaji wa sekta binafsi, biashara, uwekezaji na miradi yenye tija kwa uchumi wa Tanzania.

“Hongereni sana,” amesema Mheshimiwa Rais Mwinyi.



Akimpokea Rais tawini hapo, Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na wa Kati wa Benki ya CRDB, Muhumuliza Buberwa amesema Benki pamoja na kampuni zake tangu ni mdau mkubwa wa serikali ikijielekeza zaidi katika kuwawezesha vijana, wanawake na wafanyabiashara na wawekezaji kutimiza ndoto zao hali inayochangia kuleta matokeo chanya katika kuongeza ajira na kuinua kipato cha wananchi.

Buberwa amesema ushiriki wa Benki ya CRDB katika Maonyesho hayo ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam ni sehemu ya utekelezaji wa dhamira ya kuendelea kusogeza huduma za fedha karibu zaidi na wananchi na kuhamasisha matumizi ya huduma za kidijitali zinazorahisisha biashara na uwekezaji.

“Katika tawi hili tunawahudumia wazawa na wageni waliokuja kushiriki maonyesho haya. Katika huduma zetu sasa hivi mteja anaweza kuweka alama zake za vidole na akakamilisha muamala anaoutaka bila kulazimika kujaza karatasi. Hii ni kati ya teknolojia mpya inayolinda mazingira huku ikirahisisha huduma,” amesema Buberwa.

Katika kipindi chote cha maonesho hayo, maelfu ya wananchi walitembelea banda la Benki ya CRDB kupata elimu kuhusu bidhaa na huduma mbalimbali za benki, ikiwemo SimBanking, mikopo kwa wafanyabiashara na wajasiriamali, huduma za uwekezaji, bima, pamoja na suluhisho za malipo kwa njia za kidijitali zinazolenga kuongeza ufanisi wa shughuli za kiuchumi.

Benki ya CRDB imeeleza kuwa itaendelea kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kutekeleza ajenda za maendeleo kupitia huduma bunifu za fedha, uwekezaji katika sekta mbalimbali za uzalishaji na kuwawezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika ukuaji wa uchumi wa taifa.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments