HomeHabariWataka Katibu Mkuu CHADEMA kuunda tume ya uchunguzi

Wataka Katibu Mkuu CHADEMA kuunda tume ya uchunguzi

Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Chadema Kanda ya Kati (Mikoa ya Morogoro, Dodoma na Singida), Aquline Claud, amemuomba Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika, kuunda tume huru kuchunguza tuhuma juu ya Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho, John Heche.

Akizungumza na Waandishi wa habari, Mzee Claud amesema si vizuri kupuuzia malalamiko ya ubadhilifu w afedha yanayotajwa kwa kuwa chama hicho kimebeba imani kubwa ya wananchi wanaotaka mabadiliko.

Amesema Chama cha hakina pesa, watu wanajichanga kutoka mfukoni kwa ajili ya kukiendesha chama hicho hivyo inapotokea hela inatumika binafsi inalete mashaka na kuwatia wasiwasi wananchi na wadau wengine wa chama hicho.

“Lazima na sisi wenyewe tujisafishe. Katibu Mkuu aunde tume ambayo itafanya kazi huru, lakini kwanza anayetajwa (Heche) anayehusika akae pembeni kupisha tume ifanye kazi yake,” amesema Mzewe Claud.

Aidha, amewataka wanaharakati wanapambania mabadiliko na haki waungane na chama hicho kuunganisha nguvu katika kudai mabadiliko.

“Watu wasifanye harakati za peke yao.., Chadema ni chama chenye kudai haki, niwaombe watanzania hususani wanaharakatikuungana na chama chetu kuda mabadiliko,” amesema.

Mmoja wa wanaharakati na mwanasheria hapa nchini, Regina Donald, amesema kuungana kudai haki inategema na mitazamo.

“Ni lazima kwanza mitazamo iwe sawa ndipo watu wanapoweza kuungana…, lakini pia kuna njia nyingi inategemea huyo mwanaharakati ana lengo lipi,” amesema.

Kwa wiki kadhaa sasa baadhi ya wanachama wa Chadema wamekuwa wakijitokeza kulalamikia vitendo vya ubadhirifu wa fedha unaotajwa kufanywa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments