HomeElimuWalimu Sekondari Manispaa ya Kibaha wapewa mbinu kuondoa zero

Walimu Sekondari Manispaa ya Kibaha wapewa mbinu kuondoa zero

Afisa Elimu Mkoa wa Pwani Jimmy Nkwamu amesema jukumu la walimu ni kuhakikisha wanasaidia wanafunzi wenye ufaulu wa chini wanainuka kitaaluma na kupata wastani mzuri kwenye matokeo mengine.

Ameyasema hayo wakati wa mafunzo yaliyowakutanisha walimu wa shule za sekondari za serikali ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha Manispaa ya Kibaha lnaondoa zero kwenye shule zake.

Amesema juhudi zilizofanywa na walimu katika mitihani iliyopita na kuleta ufaulu mzuri bila kuwepo na daraja sifuri zinatakiwa kufanyika katika mitihani ya kidato cha pili na nne.

Nkwamu amemshukuru Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Dk. Rogers Shemwelekwa kwa kuwakutanisha walimu kwa pamoja katika mafunzo hayo ambayo yatasaidia pia kubadilishana uzoefu.

Afisa elimu huyo amesema anatarajia kutembelea Halmashauri zote za Mkoa wa Pwani ili kuzungumza na walimu wa Shule za Msingi na Sekondari kujadiliana mambo mbalimbali ikiwemo kukuza ufaulu.

Naye Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Kibaha Theresia Charles amewataka walimu hao kufuata na kutilia mkazo mafunzo waliyopewa na wawezeshaji ambayo yatakuwa na tija na matokeo iwapo yatatekelezwa.

Theresia amesema, awamu hiyo ni ya tatu wanakutana na wanatarajia kukutana tena kwa awamu nyingine na kuelezana mikakati ya namna ya kufanikisha Wilaya ya Kibaha na Mkoa wa Pwani kiujumla kung’ara kwenye matokeo ya kidato cha nne na cha sita.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments