HomeHabariMradi wa CREATE wabadili mafunzo ya kilimo  kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi

Mradi wa CREATE wabadili mafunzo ya kilimo  kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi

Mabadiliko ya tabianchi yameendelea kuathiri sekta ya kilimo nchini ambapo katika kukabiliana na changamoto hiyo, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) linatekeleza mradi wa Climate Change Resilience for Tanzania’s Agricultural VET Ecosystem (CREATE) unaolenga kuboresha mafunzo ya kilimo nchini.

‎‎Akizungumza kuhusu mradi huo leo Agosti 4,2026 Mtaalamu wa Miradi – NACTVET, Christopher  Majigo, amesema mradi unafadhiliwa na Umoja wa Ulaya na unatekelezwa kwa ushirikiano na taasisi kutoka Hispania, Italia na Ubelgiji, huku NACTVET ikiwa kiongozi wa utekelezaji nchini Tanzania.

‎‎”Kwa sasa mradi huu unatekelezwa katika Chuo cha Kilimo na Mifugo Kilacha mkoani Kilimanjaro pamoja na Chuo cha Kilimo Dabaga mkoani Iringa, ambavyo vitatumika kama mfano wa kueneza mafanikio hayo katika vyuo vingine vya kilimo nchini,”amesema.‎‎

Kwa mujibu wa Majigo amesema moja ya mafanikio ya mradi huo ni kuwajengea uwezo wakufunzi kupitia mafunzo yaliyotolewa nchini Italia na Ubelgiji, ambapo walijifunza mbinu za kisasa za kilimo kinachostahimili mabadiliko ya tabianchi ili kuzihamishia kwa wanafunzi na wakulima nchini..‎

Mbali na maboresho ya mitaala, mradi huo umeandaa kozi fupi tano zitakazotumiwa na walimu, wanafunzi na vyuo vinavyotoa mafunzo ya kilimo na mifugo, hatua inayotarajiwa kuongeza ujuzi wa vitendo katika sekta hiyo.‎‎

Majigo amesema mradi huo wa miaka mitatu ulioanza mwaka 2025 na unatarajiwa kukamilika mwaka 2027 pia unalenga kuwajengea vijana uwezo wa kujiajiri, sambamba na kuwaandaa kwa ajira kupitia matumizi ya teknolojia na mbinu za kisasa za kilimo.‎‎

“Vyuo vinavyoshiriki vimeanza kunufaika na vifaa vya kisasa vya kufundishia na kujifunzia, vinavyotarajiwa kuongeza ubora wa mafunzo na kuzalisha wahitimu wenye uwezo wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi katika sekta ya kilimo,”amesema.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments