HomeHabariRais Samia aitunuku PSSSF tuzo kwa kuunga mkono Ajenda ya nishati Safi...

Rais Samia aitunuku PSSSF tuzo kwa kuunga mkono Ajenda ya nishati Safi ya Kupikia

Zanzibar, Agosti 12, 2026 — Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameutunuku Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) tuzo ya kutambua mchango wake katika kuwezesha Mdahalo wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia uliofanyika Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.

Tuzo hiyo imekabidhiwa kwa Meneja wa PSSSF Zanzibar, Mariam Saleh, kwa niaba ya Mfuko, ikiwa ni sehemu ya utambuzi kwa taasisi na wadau walioshiriki kufanikisha mdahalo huo uliofanyika usiku wa kuamkia leo, Agosti 12, 2026. Mdahalo huo ulifuatiwa na Maonesho ya Picha za Tamasha la Kizimkazi.

Mdahalo huo umefanyika sambamba na Tamasha la 10 la Kizimkazi (Kizimkazi Festival 2026), linalofanyika Mkoa wa Kusini Unguja. Tamasha hilo limeanza rasmi leo kwa matembezi pamoja na uzinduzi uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Afisa Uhusiano Mkuu wa PSSSF, Fatma Elhady, amesema ushiriki wa Mfuko katika mdahalo huo unaakisi dhamira ya PSSSF ya kushirikiana na Serikali, taasisi na wadau mbalimbali katika kuunga mkono mijadala yenye umuhimu kwa jamii, mazingira na maendeleo endelevu kupitia sera ya Mfuko ya Kuwekeza kwa Jamii (Corporate Social Investment – CSI).

“PSSSF inawakaribisha wanachama na wananchi kutembelea banda la Mfuko katika Maonesho ya Tamasha la Kizimkazi yaliyoanza leo, Agosti 12, 2026, kwa ajili ya kupata elimu na huduma mbalimbali zinazotolewa na Mfuko,” amesema Elhady.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments