HomeMichezoDk. Samia ampongeza Mtanzania aliyetwaa ubingwa wa Gofu Kimataifa

Dk. Samia ampongeza Mtanzania aliyetwaa ubingwa wa Gofu Kimataifa

Rais Samia Suluhu Hassan amempongeza mchezaji wa Klabu ya Gofu ya Lugalo, Hawa Wenyeche, kwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya Uganda Ladies Open, yaliyoshirikisha wachezaji kutoka Tanzania, Ghana, Japan, Kenya, Rwanda na wenyeji Uganda.

Rais Samia amesema ushindi huo ni fahari kwa Tanzania na unaonesha uwezo wa wanamichezo wa nchini kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa.

“Ushindi huu ni fahari kubwa kwa Taifa letu na unaonesha uwezo wa wachezaji wetu kufanya vizuri katika mashindano,” ameandika Rais Samia katika akaunti yake ya mtandao wa kijamii.

Amesema Serikali itaendelea kuimarisha na kuendeleza michezo nchini kwa kuweka mazingira bora kwa wanamichezo, pamoja na kuwawezesha kushiriki na kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa.

Kwa upande wake, Wenyeche amewashukuru Watanzania kwa kumuunga mkono pamoja na timu aliyoiongoza katika mashindano hayo, akisema ushindi huo haukuwa rahisi kutokana na ushindani mkubwa uliokuwepo.

“Asanteni kwa sapoti yenu. Najua mlikuwa mnafuatilia katika mitandao na mwisho wa siku tumelichukua, na tuzo tunairudisha nyumbani,” amesema Wenyeche.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments