HomeAfyaMUHAS: Ubunifu wa vijana wazalisha suluhisho za afya na maisha ya kila...

MUHAS: Ubunifu wa vijana wazalisha suluhisho za afya na maisha ya kila siku

Tanga: Ubunifu wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) umeendelea kuvutia wananchi na wanafunzi wanaotembelea banda la chuo hicho katika Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu inayoendelea katika Shule ya Sekondari Usagara, Tanga.

Kupitia bunifu hizo, vijana wanaonyesha namna elimu, teknolojia na ubunifu vinavyoweza kubadilisha maisha ya jamii kwa kutatua changamoto zinazowakabili wananchi katika afya, mawasiliano, kilimo na usalama.

Miongoni mwa bunifu zinazoonyeshwa ni:

🔹 ROBOSPINE – Alexander Tilya
Kifaa cha roboti kinachosaidia watoto wenye spina bifida kusimama, kutembea na kufanya mazoezi, huku kikifuatilia maendeleo yao wakati wa tiba.

🔹 BiliMeasure – Abubakar Victor
Kifaa kinachowezesha upimaji na ufuatiliaji wa kiwango cha bilirubin kwa watoto wachanga wenye manjano bila kuchomwa sindano au kuchukuliwa damu wakati wa matibabu ya phototherapy.

🔹 SikuSmart – TulinaveAroha Charity
Kifaa cha kielektroniki kinachosaidia kutabiri mzunguko wa hedhi na kipindi cha yai kupevuka bila kutegemea simu janja, programu za simu au intaneti. Ubunifu huo unaweza kuwasaidia wanawake na wasichana katika maeneo yenye upatikanaji mdogo wa teknolojia ya kidijitali.

🔹 Bridging Silence – Junior Marandu
Mradi unaotumia Akili Bandia (AI) kutambua lugha ya alama na kuibadilisha kuwa maandishi na sauti ya Kiswahili, kwa lengo la kurahisisha mawasiliano kati ya watu wanaotumia lugha ya alama na wasioifahamu.

🔹 BioSafe – Zaituni Msengwa
Kiuatilifu hai cha asili kinacholenga kudhibiti vimelea vya magonjwa ya mimea, kuongeza uzalishaji na ubora wa chakula, huku kikisaidia kupunguza matumizi ya viuatilifu vya kemikali na kulinda mazingira pamoja na afya za watumiaji.

🔹 MoyoGuard – Staphod Mwahalende
Kifaa cha mkononi kinachorekodi mapigo ya moyo ndani ya sekunde 30 bila kuhitaji intaneti. Teknolojia hiyo huchanganua mapigo ya moyo na kusaidia kutambua mabadiliko yasiyo ya kawaida ili hatua zichukuliwe mapema.

🔹 QR Dharura – Pharm Flavian Sanga
Msimbo wa QR unaoweza kuwekwa kwenye begi la shule, sticker ya helmeti au kamba ya mkononi ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa muhimu za mtu wakati wa dharura.

Maadhimisho hayo yanaendelea hadi Agosti 24, 2026, huku MUHAS ikiendelea kuwahamasisha vijana kuona kuwa elimu si darasani pekee, bali ni nyenzo ya kubuni majibu ya changamoto zinazowakabili watu katika maisha ya kila siku.

MUHAS #Ubunifu #ElimuNaUbunifu #Tanga #Teknolojia #Vijana #Afya #Innovation

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments