HomeHabariDk. Samia: Tumieni busara kuwaondoa wamachinga barabarani

Dk. Samia: Tumieni busara kuwaondoa wamachinga barabarani

Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amewataka wakuu wa mikoa kuweka utaratibu mzuri wa kuwaondoa wafanyabiashara wadogo wanaofanya shughuli zao katika maeneo yasiyo rasmi na kuwawezesha kurejea katika masoko yaliyotengwa.

Rais Samia amesema Serikali imefanya kazi kubwa ya kujenga masoko ya kisasa, lakini wafanyabiashara wadogo wameanza kurejea kwa kasi katika maeneo ya mbele ya maduka na mitaani.

Amesema hayo jana, Septemba 2, 2026, wakati akiwaapisha wakuu wa mikoa na makatibu tawala aliowateua hivi karibuni katika Ikulu Ndogo ya Tunguu, Kusini Unguja.

Amesisitiza kuwa wafanyabiashara hao hawapaswi kuondolewa kwa kutumia nguvu, bali viongozi wanapaswa kuweka mipango inayowawezesha kuhamia katika masoko rasmi.

Twendeni tukayasimamia haya, si kwa kuwapiga fimbo na askari mgambo au kuwanyang’anya bidhaa zao, hapana. Bali kwa mipango mizuri, ili watoke waliko, warudi katika masoko,” amesema.

Rais Samia amewataka viongozi kutatua changamoto ndogo zinazowafanya wafanyabiashara hao kuacha masoko na kurejea mitaani.

Amesema, endapo changamoto ni usafiri, ikiwamo daladala kutofika katika maeneo ya masoko, viongozi wanapaswa kutafuta njia mbadala ili wananchi na wafanyabiashara waweze kuyafikia.

Kama ni kelele daladala hazifiki, tengenezeni njia mpya ili zikashushe. Kuna mambo madogo yanayowafanya watoke na kurudi mtaani. Nendeni mkasimamie na kujipanga vizuri. Tumerelax, tunasubiri wakubwa, ndiyo tutumie nguvu kuwaondosha,” amesisitiza.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments