Wafanyabiashara wilayani Kasulu wametakiwa kuwa mabalozi wa sheria za kodi kwa kuwafikishia wafanyabiashara wenzao elimu kuhusu umuhimu wa kutekeleza wajibu wao wa kikodi kwa usahihi na kwa wakati.
Wito huo umetolewa na Afisa Elimu kwa Mlipakodi Justine Katiti wakati akitoa elimu kwa walipakodi wa wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma juu ya mabadiliko ya sheria za kodi 2026/27




Amesema kutokana na umuhimu wa kuongeza uelewa miongoni mwa wafanyabiashara kuhusu mabadiliko ya sheria za kodi, usajili wa biashara, matumizi sahihi ya mifumo ya kielektroniki ya kodi pamoja na ulipaji wa kodi kwa mujibu wa sheria.
TRA imeendelea kusisitiza utoaji wa elimu kwa walipakodi ili kuongeza utii wa hiari na kuwawezesha wafanyabiashara kutekeleza majukumu yao kwa usahihi.





