Kwa jamii ambazo zimeishi kwa miaka mingi bila kuwa na uhakika wa upatikanaji wa maji safi na salama, kupata kituo cha maji ya kutosha kunaweza kubadilisha kwa kiasi kikubwa maisha ya kila siku. Safari iliyokuwa ikichukua masaa kadhaa inaweza kupungua na kuwa dakika chache na kutoa muda zaidi kwa familia kufanya kazi na shughuli nyingine, kuwawezesha watoto kutumia muda zaidi shuleni, na kusaidia jamii kudumisha mazingira bora na yenye afya.
Mabadiliko haya ya kila siku ndiyo yanayofanya upatikanaji wa maji safi na salama kuwa sehemu muhimu ya maendeleo, hasa katika jamii za vijijini ambako vyanzo vya maji vya uhakika bado ni changamoto ikizingatiwa kuwa kukosekana kwa maji kunatatiza afya ya jamii na usafi kwa ujumla.
Kutokana na umuhimu wa maji katika Kuadhimisha Wiki ya Maji Duniani (World Water Week), Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) inaangazia zaidi ya muongo mmoja wa kazi yake katika kuboresha upatikanaji wa maji na kuendeleza matumizi sahihi ya rasilimali za maji nchini Tanzania.
Kupitia mpango wake wa ‘Water for Life’, SBL imekuwa ikilenga kuboresha upatikanaji wa maji safi na salama katika jamii za vijijini, hususani katika maeneo ambayo upatikanaji wa vyanzo vya maji vya uhakika umekuwa changamoto. Hata hivyo, mpango huo hausishii katika uwekezaji wa miundombinu ya maji, unalenga pia kuwawezesha jamii kushiriki katika kusimamia, kutunza na kuhakikisha uwekezaji huo unaendelea kuwa na manufaa kwa muda mrefu.
Katika kipindi cha zaidi ya miaka 10, SBL imewekeza zaidi ya shilingi bilioni 2 katika miradi 32 ya maji katika mikoa zaidi ya 10 nchini Tanzania. Miradi hiyo imewafikia zaidi ya watu milioni 2.3, nakusaidia jamii kupata maji safi na salama kwa urahisi zaidi na kuweka mazingira yanayosaidia maisha yenye afya na tija.
Katika utekelezaji wa miradi ya maji, SBL imegundua kuwa kujenga kituo ni mwanzo tu. Ili uwekezaji huo uendelee kuleta matokeo, jamii inahitaji kuwa sehemu ya wamiliki, kuwa na uelewa wa namna ya kutunza rasilimali za maji na kushiriki katika kuhakikisha miundombinu inaendelea kufanya kazi.
Hii ndiyo sababu SBL imewekeza pia katika kuwawezesha wanawake mabalozi wa maji ‘Water Champions’, ambao wamekuwa sehemu muhimu ya mpango wa ‘Water for Life’. Zaidi ya wanawake 100 wamepewa elimu, maarifa na ujuzi wa kuhamasisha uhifadhi wa maji, usafi na matumizi sahihi ya maji katika jamii zao.
Mbali na kutoa elimu, wanawake hawa wanahamasisha jamii kushiriki katika kulinda vyanzo vya maji na kutunza miuondombinu inayowasaidia kupata huduma hiyo. Ushiriki wao unaifanya ‘Water for Life’ kuwa ni mpango wa kujenga vituo vya maji na uwekezaji katika uwezo wa jamii kusimamia rasilimali ambayo ni muhimu kwenye maisha yao.
Mtazamo huu ni muhimu hasa katika maeneo ya vijijini, ambako huduma za maji endelevu hautegemei miundombinu pekee. Unahitaji pia jamii inayotambua thamani ya miradi hiyo, inayoshiriki katika kuyatunza na kuhakikisha vyanzo vya maji vinalindwa.
Kwa SBL, hii ni sehemu ya safari yake pana ya uendelevu na dhamira ya kuwa mshirika anayewajibika katika jamii anazofanya nazo kazi. Utunzaji wa maji unahitaji ushirikiano wa muda mrefu kati ya sekta binafsi, serikali na jamii, pamoja na suluhisho zinazoweza kuendelea kuleta manufaa hata baada ya mradi kukamilika.
Takwimu zinaelezea sehemu ya hadithi yake: zaidi ya miaka 10 ya uwekezaji, miradi 32 ya maji, katika zaidi ya mikoa 11, zaidi ya kiasi cha shilingi bilioni 2 zilizowekezwa na kusaidia watu zaidi ya milioni 2.3.
Thamani ya uwekezaji huu inaonekana zaidi pale tunapoangalia kinachotokea baada ya maji kufika. Kwa baadhi ya jamii, upatikanaji wa maji karibu unawawezesha watu kuelekeza muda mwingi kwenye shughuli zao za kila siku. Kwa wanawake waliowezeshwa kuwa ‘Water Champions’, jukumu linaenda hatua moja zaidi; wanakuwa sehemu ya juhudi za kuhamasisha usafi, matumizi sahihi ya maji na utunzaji wa vyanzo vya maji katika jamii zao.
Hii ndiyo maana ya SBL, ‘Water for Life’ haijawa tu kuhusu kujenga au kukarabati miundombinu ya maji. Kwa zaidi ya muongo mmoja, mpango huu umeendelea kuunganisha uwekezaji katika miundombinu na uwezeshaji wa jamii, kwa kutambua kwamba huduma ya maji yenye manufaa ya muda mrefu inahitaji jamii inayoshiriki katika kuilinda na kuitunza.
Kutoka kwenye mradi mmoja hadi mingine, kutoka kwenye miradi 32 katika zaidi ya mikoa 11 hadi kuwafikia zaidi ya watu milioni 2.3, safari hii imeendelea na kuwa zaidi ya kujenga vituo vya maji kwani inajenga pia ushiriki wa jamii katika kutunza rasilimali ambayo maisha yao yanaitegemea.
Na hapo ndipo maana ya uwekezaji wa SBL katika maji unapojitofautisha kwani si tu wanaongeza upatikanaji wa maji, bali kusaidia kuhakikisha uwekezaji huo unaendelea kuwa na thamani kwa jamii zinazoutegemea leo na katika miaka ijayo.





