Makamu wa Rais, Deogratius Ndejembi, ameapishwa kushika wadhifa huo rasmi, siku tatu baada ya jina lake kupendekezwa na kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
Jina la Ndejembi, lilipendelezwa Agosti 26, 2026 na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Dk Emmanuel Nchimbi, aliyejiuzulu na baadaye kufukuzwa uanachama wa CCM.


Jana, Agosti 28, 2026 jina la Ndejembi lilipelekwa bungeni na kuthibitishwa kwa kura za ndio 329 sawa na asilimia 100 ya wabunge waliokuwepo bungeni.
Ndejembi, ameapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, George Masaju leo, Agosti 29, 2026 Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma, tukio lililoshuhudiwa na Rais Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine wa Serikali.





