Makamu wa Rais, Deogratius Ndejembi, ameapishwa kushika wadhifa huo rasmi, siku tatu baada ya jina lake kupendekezwa na kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
‎Jina la Ndejembi, lilipendelezwa Agosti 26, 2026 na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Dk Emmanuel Nchimbi, aliyejiuzulu na baadaye kufukuzwa uanachama wa CCM.


‎Jana, Agosti 28, 2026 jina la Ndejembi lilipelekwa bungeni na kuthibitishwa kwa kura za ndio 329 sawa na asilimia 100 ya wabunge waliokuwepo bungeni.
‎Ndejembi, ameapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, George Masaju leo, Agosti 29, 2026 Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma, tukio lililoshuhudiwa na Rais Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine wa Serikali.





