Wednesday, February 4, 2026
spot_img
HomeHabariRais wa TAHLISO afanya ziara na kuwasilisha changamoto za wanafunzi kwa NACTVET

Rais wa TAHLISO afanya ziara na kuwasilisha changamoto za wanafunzi kwa NACTVET

Dar es Salaam, 6 Mei 2025 — Rais wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu nchini (TAHLISO), Geofrey Kiliba, amefanya ziara rasmi katika Ofisi za Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) kwa lengo la kuwasilisha changamoto mbalimbali zinazowakabili wanafunzi wa vyuo vya kati na vyuo vya ufundi nchini.

Ziara hiyo ameifanya leo kufuatia kukamilika kwa mfululizo wa ziara alizozifanya katika mikoa mbalimbali, ambako alipata nafasi ya kusikiliza na kukusanya maoni na changamoto kutoka kwa wanafunzi katika taasisi mbalimbali za elimu ya juu.

Katika ziara hiyo, Rais Kiliba alipokelewa na Katibu Mtendaji wa NACTVET, Dk. Mwajuma, pamoja na ujumbe wake wa viongozi waandamizi wa Baraza hilo. Mazungumzo yao yalilenga kuimarisha ushirikiano baina ya TAHLISO na NACTVET katika kushughulikia masuala ya msingi yanayowahusu wanafunzi, hususan yanayohusiana na ajira baada ya kuhitimu, ubora wa mafunzo kwa vitendo, usimamizi wa mitaala, na uboreshaji wa mazingira ya kujifunzia.

Rais Kiliba amesisitiza dhamira ya TAHLISO katika kuendeleza ushirikiano na taasisi za Serikali ili kuhakikisha kuwa sauti ya mwanafunzi inasikika na changamoto zake kutatuliwa kwa wakati. Aidha, Dk. Mwajuma amepongeza juhudi hizo na kuahidi kuwa Baraza litaendelea kushirikiana kwa karibu na TAHLISO katika kuhakikisha elimu ya ufundi nchini inakuwa chachu ya maendeleo ya Tanzania.

Previous article
Next article
Wanafunzi TUSIIME kufundishwa Artificial intelligence AI Na Mwandishi WetuKATIKA jitihada za kuendana na mtaala mpya wa elimu uliozinduliwa hivi karibuni na Serikali, unaojumuisha Mahili 11 yanayolenga kuendeleza ujuzi na stadi kwa wanafunzi, shule za Tusiime zimechagua program za Kompyuta kama kipaumbele chao.“Tukiwa na dira ya kuandaa wanafunzi kwa maisha ya kesho yanayotawaliwa na teknolojia, hususan katika zama hizi za akili mnemba Artificial Intelligence (AI), shule zetu za Tusiime kuanzia shule ya awali, msingi na sekondari mpaka kidato cha sita zimeanza rasmi utekelezaji wa somo la Introduction to Complete Programming kwa wanafunzi wa ngazi mbalimbali,” amesema leo Mkurugenzi wa shule hizo, Dk Albert Katagira.Alisema lengo la kuanza kufundisha program za kompyuta ni kuhakikisha kuwa wakifika kidato cha sita, kila mwanafunzi wa Tusiime awe na ujuzi mpana wa kujua program mbalimbaali za kompyuta.Dk Katagira alisema mafunzo hayo yatamwezesha mwanafunzi kujiajiri kupitia utengenezaji wa programu rahisi, kuunda vikundi vya programmer rika (peer programming groups), kushiriki kwenye miradi ya pamoja ya teknolojia na kutengeneza suluhisho za kidigitali kwa changamoto za kijamii na kiuchumi. “Kwa sasa, mafunzo ya awali yameshaanza kwa vitendo, ambapo wanafunzi wetu wa shule ya msingi tayari wanafundishwa msingi wa programming, ikiwemo kutumia lugha kama Scratch na Python (kwa baadaye),” amesema na kuongeza.“Kwa kutambua umuhimu wa ushirikiano na jamii, hususan wazazi, shule za Tusiime inatekeleza kampeni ya uhamasishaji ili kutoa uelewa kwa wazazi kuhusu faida za mahili ya Programming,” amesemaAidha, amesema shule hizo zinatoa nafasi kwa wadau mbalimbali kushirikiana nao katika safari hii ya mapinduzi ya elimu, kuandaa wanafunzi wanaoweza kuhimili ushindani wa soko la ajira la kidigitali.“Tunawaalika wazazi, wadau wa elimu na jamii kwa ujumla kuunga mkono juhudi hizi katika kuwajengea vijana wetu msingi imara wa mafanikio ya baadaye kwasababu shule za Tusiime tunajenga kizazi cha kesho chenye maarifa, ujuzi na ubunifu,” amesema Dk Katagira.
RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments