Mgombea udiwani kata ya Masama Kusini wilayani Hai Mkoa wa Kilimanjaro,Cedrick Pangani kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), amechukua fomu ya kuwania kiti hicho kwa mara ya pili katika ofisi ya mtendaji kata.

Pangani ambaye alisindikizwa na mke wake Janeth Pangani pamoja na wananchi wa kata hiyo ametumia nafasi hiyo kuwaahidi wananchi hao endapo watamchagua kwa kipindi kingine Masama Kusini itakuwa ni kata ya mfano Wilaya ya Hai.
“Mkinipa ridhaa kwa mara nyingine kata yetu hii itakuwa ni ya mfano, kwa kata nyingine kuja kujifunza kwetu kwa maandeleo tuliyonayo, pia mkininga mkono nitahakikisha naendeleza na kumaliza kazi zote nilizokuwa nimezianza katika kipindi kilichopita.” amesema
Pia amewataka wananchi wa kata hiyo kuendelea kushirikiana kuhakikisha kata hiyo inazidi kupiga hatua katika maendeleo.







